Waziri Ummy-Hospitali za serikali pimeni saratani kizazi na matiti kila mwezi...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Salha Mohamed
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amezitaka hospitali, zahanati na vituo vya
afya ngazi ya wilaya kila mwezi kutenga
siku moja kupima saratani ya shingo ya
mlango wa kizazi na matiti.
Waziri Ummy Mwalimu akihutubia mara baada ya kumaliza matembezi ya kuhamasisha upimaji na kuchangia damu kwa wagonjwa wa saratani jijini Dar es salaam leo
Wito
huo ameutoa leo jijini Dar es Salaam
mara baada ya kuhitimisha matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi
wa saratani ya matiti na saratani ya shingo ya mlango wa kizazi katika viwanja
vya Taasisi ya saratani Ocean Road.
Amesema ugonjwa wa
saratani unaongezeka kila takwimu za wizara ya Afya zinapotolewa na kila
mwaka kuna wagonjwa wapya wa saratani 50,000.
"Ikifika
2020 wagonjwa na vitu vitokanavyo na
saratani vitaongezeka mara mbili ya wagonjwa wapya na kufikia wagonjwa 100,000
kama hatua hazitachukuliwa, "amesema.
Waziri
Ummy amesema kutokana na takwimu hizo ni asilimia 26 ya wagonjwa ndiyo hufika
hospitali kwa ajili Uchunguzi wa saratani.
Amesema
katika wagonjwa 100 wagonjwa 74 hawajulikani wanapopata tiba na uchunguzi huku
asilimia 80 ya wagonjwa hufika wakiwa katika hatua za mwisho na kusababisa
matibabu kutokuwa mazuri.
"Saratani
tunaweza kushindwa, leo tumetembea
kuonesha hamasa na tumeokoa maisha ya watu wengi na serikali imeandaa mkakati
wa kuondoa saratani kabisa, "amesema Waziri Ummy.
Ameongeza
awali upatikanaji wa dawa ulikuwa asilimia 4 tu kutokana na bajeti ndogo
nakusababisha upatikanaji wake kuwa mgumu kwa kupokea milioni 790 kwa mwaka
2005/2017 lakini bilioni 7 kwa mwaka
2016/2017 zimetolewa.
Amesema
kutokana na ukubwa wa tatizo serikali itashusha zaidi dawa ili kutibu wagonjwa
wengi zaidi.
Amesema
kwa sasa mgonjwa anatakiwa kupata huduma ya matibabu ndani ya wiki mbili na si
wiki sita kama ambayo Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Dk. Julius
Mwaiselage alivyosema.
Ummy
amesema serikali inataka hadi kabla ya June 30, 2018 kuwa na kipimo cha kisasa Afrika Mashariki
kwani itapunguza wagonjwa wa nje kwa kufuata kipimo cha PET/CT Scan ambapo
imetoa bilioni 14.5.
Amesema
hadi kufikia Desemba 2018 wawe wamepima wagonjwa 3,000,000 pamoja na kutoa
elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi.
Kwa
upande wake Dk Mwaiselage amesema saratani ikiwahi kutibiwa inatibika na kuwa
elimu zaidi inahitajika.
"Mashine
mbili mpya zitafungwa na itapunguza muda wa kusubiri tiba na hata wanaotaka
kwenda nje ya nchi, "amesema.
Ameongeza
kupitia matembezi hayo wameboresha wodi ya Chemotherapy(tiba kwa drip) kutoka vitanda 40 hadi 100.
No comments:
Post a Comment