Shindano vipaji vya sauti 10 wapatikana..Soma habari kamili na Matukio360..#share
SHINDANO linalodhaminiwa na kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia StarTimes na chaneli yake ya Star Swahili la kusaka vipaji vya sauti kwa msimu wa pili limefikia tamati usiku wa kuamkia leo huku washindi 10 wakipatikana kwa ajli ya kwenda nchini China.
Miongoni mwa watu walioibuka washindi ni Msanii wa filamu Bongo, Koletha Raymond, aliyeibuka mshindi namba moja baada ya kuwabwaga washiriki zaidi ya 25, aliokuwa akichuana nao kwa ajili ya kuwania nafasi ya kwenda kufanya kazi makao makuu ya Kampuni ya Star Times, nchini China kuigiza sauti ya filamu mbalimbali zilizochezwa kwa lugha mbalimbali.
Shindano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam na kupatikana washindi 10, wataungana na Koleta kwenda nchini humo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo ambayo wataifanya kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Washindi hao wamepatikana katika ushindani mkali mbele ya majaji watatu wakiongozwa na wasanii Jacob Steven ‘JB’ na Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ ambapo haikuwa kazi rahisi kwa majaji hao na washiriki wenyewe kutokana na ushindani mkali uliojitokeza.
Washiriki 25, watano kutoka Mwanza, watano kutoka Zanzibar na 15 wa Dar es Salaam, walichuana vikali kupata washindi 10 wanaokwenda kufanya kazi hiyo nchini China.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili kwa mwaka 2017.
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza na waandishi wa habari wakati wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili mwaka 2017 lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti walioshinda kwenda nchini China kufanya kazi makao makuu ya Kampuni ya Startimes kwenye fainali iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Washindi hao ukianzia kushoto ni katika picha ya pamoja hapo juu ni 1: Coletha Raymond, 2: Hosea Joel, 3: Bakari Hassan Masasi, 4: Alex Herbert, 5: Doreen Aurelian Ponera, 6: Hamza Tambwe, 7: Jacqueline F. Shuma, 8: Alli Ahmed Shani, 9: Mathias Komba, 10: Mustapha Mussa Senzia
Mmoja wa washindi walioingia kumi bora akipokea zawadi ya simu ya Startimes kutoka kwa Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif mara baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi (kulia) akimkabidhi zawadi ya Television ya StarTimes mshindi wa kwanza wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili, Coletha Raymond mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa shindano hilo.
Mshindi wa kwanza hadi wa tatu wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili mwaka 2017 wakiwa kwenye picha ya Pamoja.
No comments:
Post a Comment