Lukaku avunja rekodi upachikaji mabao timu ya taifa...soma habari kamili na Matukio360..#share
Timu ya Ubelgiji inayofundishwa na Roberto Martinez waliifunga jana
Japan bao 1-0 huko Brugge.
Lukaku, 24, alifunga goli hilo na kufikisha mabao 31 akiwa
mchezaji wa kikosi hicho.
Mshambuliaji huyo alimalizia
krosi safi kutoka kwa Nacer Chadli aliyoiingiza wavuni kwa kutumia kichwa.
Kabla ya kufunga goli hilo, Lukaku alikuwa sawa na wachezaji Bernard Voorhoof na Paul van
Himst kwa kuwa na magoli 30 kila mmoja.
Ubelgiji waliendeleza msururu wao wa kutoshindwa hadi mechi 15.
Mara yao ya mwisho kushindwa ilikuwa mikononi mwa Uhispania
mechi ya kirafiki Septemba 2016.
Katika michezo mingine iliyochezwa jana, Uholanzi walipata
ushindi wao wa pili tangu kukosa nafasi ya kushiriki katika Kombe la Dunia
nchini Urusi walipopokeza Romania kichapo cha magoli 3-0 huko Bucharest.
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Ryan Babel alifunga bao lake
la kwanza la kimataifa tangu mwezi Mei 2008, pamoja na mchezaji mwenza Memphis
Depay na Luuk de Jong.
Mabingwa wa Euro 2016 Ureno walitoka sare 1-1 na Marekani,
wakicheza bila nyota wao Cristiano Ronaldo. Vitorino Antunes alikomboa bao
lililokuwa limefungwa na Mmarekani Weston McKennie mapema mwenye mechi Leiria.
No comments:
Post a Comment