Ununuzi nyumba za Lugumi utata!...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
UTATA
umegubikwa kuhusu ununuzi wa nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi zilizouzwa
kwa njia ya mnada hivi karibuni.
Moja ya nyumba ya mfanyabiashara, Said Lugumi iliyouzwa hivi karibuni kwa njia ya mnada
Habari zilizopatikana ni kuwa mnunuzi wa
nyumba hizo Dk Luis Shika amedaiwa kuwa ni tapeli na kwamba inadaiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Hata
hivyo kamanda wa polisi kanda maalumu ya
Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa leo
ameiambia Matukio360 kuwa hana habari za kukamtwa kwa mununuzi huyo, Dk Shika
"Hadi
muda huu(saa nane na nusu mchana) bado sijapata taarifa zozote kuhusu kukamatwa
kwa huyo mnunuzi. Natumai hadi kesho ninawezakuwa na taarifa kamili kuhusu
hilo," amesema Mambosasa
Inadaiwa
kuwa nyumba ya Lugumi iliyopo JKT Mbweni imenunuliwa kwa bilioni 1.1 na
nyingine kwa bilioni 1.
No comments:
Post a Comment