'UPDATES' Mtoto wa Chacha Wangwe jela mwaka mmoja na nusu...soma habari kamili na Matukio360..#sgare
Na Abdulrahim Sadiki
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi
Kisutu leo imemtia hatiani na kumuhukumu
kwenda jela mwaka mmoja na nusu au kulipa faini ya milioni tano, BOB Chacha Wangwe ambaye ni mtoto
wa mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Hatua hiyo inafuatia baada ya hakimu Mkazi
Mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi kuridhika na ushahidi uliotolewa kuwa Bob
Chacha kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii
Upande wa Mashtaka
uliwaita mashahidi sita kutoka ushahidi kwenye kesi hiyo na mshtakiwa huyo kujitetea
mwenyewe
Kwa
mujibu wa kesi hiyo namba 167, 2016
ambayo ilifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 12,2016.
Bob Chacha Wangwe ambaye kitaaluma ni mwana sheria na
mwanaharakati wa haki za binadamu anadaiwa kutenda kosa la
kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa Facebook.
Mshtakiwa
huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Machi 15,2016 na kwamba alichapicha maneno
haya; “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka
Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya
Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”
No comments:
Post a Comment