‘UPDATES’ Wapigania uhuru Zimbabwe wampa siku tatu Mugabe ajiuzulu urais..soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
SAA chache baada chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF kimemfuta
Robert Mugabe kama kiongozi wake na Grace Mugabe ambaye alikuwa mwenyekiti wa
taifa wa wanawake, wapigania uhuru wa nchi hiyo wamempa siku tatu Mugabe
ajiuzulu urai kwa hiari yake.
Msimamo huo umetangazwa leo muda huu na mkuu wa chama chenye nguvu cha
wale waliopigania uhuru, Chris Mutsvangwa.
Ameiambia Reuters kuwa chama
kinaanza mchakato wa kumuondoa Mugabe
madarakani kama rais endapo atakataa kujizulu mwenyewe.
"Tumempa siku tatu
ajiuzulu mwenyewe akishindwa kutekeleza hilo, tutamtoa kwa nguvu,’’ amesema Chris Mutsvangwa..
Zanu-PF ndio chama
kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40.
Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia
mpasuko mkubwa katika chama tawala.
Pia Zanu-PF kimemfuta waziri wa elimu Jonathan Moyo na waziri wa serikali za mitaa,
Saviour Kasukuwere
Kimemteua aliyekuwa makamu wa rais, Emmerson Mnangagwa
ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi wake.
Hata hivyo kufutwa kwa Mnangawa kumezua mambo mengi huku jeshi
likitwaa madaraka na kumzuia Mugabe mwenye umri wa miaka 93, kumteua mke wake,
Grace kama makam wa rais.
Jana waandamanaji walipiga
kambi nje ya makao ya Mugabe kumshinikiza kujiuzulu
Maelfu ya watu nchini
Zimbabwe waliingia barabarani siku ya Ijumaa kuandamana kumpinga Mugabe.
Mugabe anatarajiwa kukutana
na makanda wa jeshi na msafara wa magari umeonekana ukiondoka makao ya rais.
Jeshi la nchi hiyo
lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani
tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina.
Mugabe angependelea mkewe
kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa
Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na
uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa
madaraka.
No comments:
Post a Comment