Nyalandu, Mbowe waunguruma Mwanza...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Chadema,  Freeman Mbowe na aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu wapo jijini Mwanza  kwa nyakati tofauti wamehutubia katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa uchaguzi mdogo wa udiwani  kumnadi mgombea wa chama hicho, utakaofanyika Novemba 26, 2017.

Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Lazaro Nyalandu akiwa katika mkuatano wa hadhara 

Wapo kumnadi mgombea  udiwani wa chama hicho, Godfrey Misana  ambaye yupo mahabusu akikakabiliwa na  shitaka la kujeruhi.

Afisa habari wa Chadema taifa, Tumaini Makene  leo ameiambia Matukio360 kuwa pamoja na kuwa Nyalandu bado hajapokea rasmi kadi ya kujiunga na  Chadema lakini anaruhusiwa kukinadi chama hicho.

"Mbali na Mbowe hivi sasa Nyalandu yupo jukwaani akimnadi mgombe udiwani wa Chadema japo bado hajapata kadi rasmi ya kujiunga na chama," amesema Makene

Amesema mkutano huo pia utahudhuriwa na aliyekuwa mbuge wa Nyamagana, Ezekia Wenje na utafanyika saa kumi jioni.

Misana (46), mgombea udiwani wa Chadema katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 26,2017 na kampeni meneja wake, Charles Chinjibela (37) Ijumaa Novemba 17,2017 walipandishwa kizimbani wakidaiwa kumjeruhi meneja wa kampeni za CCM katika kata hiyo, Thomas Warioba.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, mbele ya hakimu Ainawe Moshi wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 14,2017.

Akisoma mashtaka katika shauri hilo namba 540/2017, mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Elizaberth Barabara alidai washtakiwa walitumia visu na mawe kumjeruhi Warioba.

Upande wa Jamhuri uliomba Mahakama kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile ilichoeleza ni kwa usalama wao.

Ombi hilo la Jamhuri limepingwa na wakili wa utetezi, Gasper Mwanaliela.

Wakili Mwanaliela alisema dhamana ni haki ya wateja wake na kwamba, kuwanyima kutawazuia kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Moshi alisema Mahakama itatoa uamuzi kuhusu dhamana Novemba 21,2017. Washtakiwa walipelekwa mahabusu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search