Wawili wajiondoa kugombea udiwani ....soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
WAGOMBEA
wawili wa udiwani, Lunda Rashid Ulaya(CHADEMA) kata ya Milongodi wilayani
Tandahimba mkoani Mtwara na Juma Mohamed
Siyame wa Chama cha ACT Wazalendo kutoka
kata ya Ndalambo katika Halmashauri ya Momba. wamejiondoa katika kinyanganyiro
hicho
Watendaji wa wakuu wa NEC
Taarifa hiyo inasema
"Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeridhia kujitoa kwa wagombea wawili wa Udiwani
katika Kata ya Milongodi, Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara na
Kata ya Ndalambo katika Halmashauri ya Wilaya Momba mkoani
Songwe.
Wagombea waliojitoa ni Ndugu Lunda Rashid Ulaya wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka katika kata ya Milongodi
Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba na Juma Mohamed Siyame wa Chama cha ACT Wazalendo kutoka kata ya
Ndalambo katika Halmashauri ya Momba.
Katika
kikao cha chake kilichofanyika tarehe 14/11/2017 jijini Dar es Salaam, Tume
imeridhia uamuzi wa kujiondoa kwa
wagombea hao wawili katika nafasi ya udiwani, baada ya kukamilisha taratibu
zote za kujitoa.
Miongoni
mwa taratibu hizo ni mgombea kuandika barua kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo
au msimamizi msaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kumjulisha uamuzi wa kujitoa .
Katika
barua yake kwenda kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata, mgombea wa
kata ya Milongodi Ndugu Lunda Rashid Ulaya katika barua yake ya tarehe
4/11/2017 hakueleza sababu zilizomfanya ajitoe kwenye kinyang’anyiro hicho cha
kugombea udiwani.
Kwa
upande wake mgombea wa ACT WAZALENDO Ndugu Juma Mohamed Siyame, katika barua
yake ya tarehe 10/11/2017 alieleza sababu za kujitoa ni kuwa na majukumu ya kifamilia na hivyo
asingeweza kumudu kuwatumikia wananchi wa Ndalambo katika shughuli mbalimbali
za maendeleo.
Kutokana
na kujiondoa kwa wagombea hao, idadi ya wagombea waliobaki katika
kinyang’anyiro hicho sasa ni 151. Uchaguzi mdogo wa madiwani unafanyika katika
kata 43 ambazo ziko katika Halmashauri 36
kwenye mikoa 19 Novemba 26,
2017.
Imetolewa
leo tarehe 15 Novemba, 2017 na:-
Kailima, R.K
MKURUGENZI
WA UCHAGUZI
No comments:
Post a Comment