Achoma nyumba na kumuuwa mume wake....soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
JESHI la Polisi Mkoani Mtwara linamsaka Zuhura Ismail (29) kwa tuhuma za kumuua mume wake baada ya kumfungia ndani na kuichoma nyumba kwa petroli.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mondya.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi mkoani humo Lucas Mkondya, amesema kwamba chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi, baada ya mwanamke huyo kugundua mume wake anaishi na mke mwingine hivyo akaamua kumvizia nyumbani kwake na kuichoma moto.
"Ni kweli Jeshi la linamsaka mwanamke mmoja ayefahamika kwa jina la Zuhura Ismail kwa tuhuma za kuichoma nyumba aliyokuwa anaishi mume wake na mwanamke mwingine, kutokana na wivu wa kimapenzi baada ya Zuhura kugundua kuwa mumewe anaishi na mke mwingine," amesema Kamanda Mkondya.
Ameeleza kuwa moto huo uliwasababishia majeraha makubwa na kukimbizwa hospitali lakini kutokana na majereha hayo makubwa alifariki dunia huku mwanamke aliyekuwa nae akiendelea vizuri.
Kamanda Mkondya amesema mara baada ya tukio hilo Zuhura alitoroka na kwenda kusikojulikana na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka na pindi atakapopatikan atafikishwa katika vyombo vya sheria.

No comments:
Post a Comment