Rais Shein atoa ya moyoni....soma habari kamili na matukio360..#share


Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MAKAMO mwenyekiti CCM Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein ametoa ya moyoni na  kwamba  si mpole ila anafanyakazi kwa kufuata taratibu za chama na katiba ya nchi.

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein

Dkt. Shein ambae pia ni rais wa Zanzibar amesema hayo leo katika
hafla ya kupokewa kwake kufuatia kuchaguliwa tena kuwa makamo wa CCM kwenye uchaguzi  mkuu wa chama hicho uliofanyika Dodoma wiki iliyopita.

Amesema wanaingia  mwaka 2018 kwa  kufanya kazi kwa kauli moja  na sio kulaumiana na kupakana matope.

“Leo  napasua jipu na sikama napasua jipu kwa kuvunja utaratibu bali
napasua jipu hili la utaratibu wa chama chetu, waliokuwa hawajui na
wajuwe , nimewavumilia sana, nimestahamili sana, mimi si mpole bali
naheshimu mkubwa na mdogo na si kama hivyo mnavyonidhania”, amesema.

Amesema inafika wakati kama kiongozi wa nchi atumie busara na
sio kuchukuwa maamuzi ya kuwaadhibu watu.

 “Stahamala ina mwisho wake na mwisho wake ni mara tu baada ya kumalizika uchaguzi mkuu lakini sasa ni wakati wa ukweli na uwazi”.

Sambamba na hilo amewataka viongozi wa matawi na mashina kujitahidi
kuvitumia vikao vya chama kutoa maamuzi na sio kusubiri mwenyekiti au
makamo mwenyekiti achukuwe hatua.

Alisema kuwa CCM ni chama kikongwe ambacho kina utaratibu wake wa
kiongozi iwapo kumetokea tatizo jaribuni kulimalizia katika vikao
vyenu na sio kukaa hadi ufanyike mkutano mkuu wa chama.

“Nadhani hili si jambo geni kwetu kwani tulishawahi kutokea kiongozi
alichukuliwa hatua katika tawi lake na sisi kama viongozi wakuu
tukaweza kubariki maamuzi yao,” amesema.

Amewataka viongozi wapya ambao wamechaguliwa  kujitahidi
kufanyakazi za chama ipasavyo na kuwa na kasi na nguvu mpya ili
kufikia lengo la wananchama wao waliowachaguwa.
Amesema  kazi ya siasa kwa sasa ni lazima iwe na kasi mpya,
nguvu mpya na ari iongezeke kutokana na kuwa ni ya ushindi na hawana
mbadala na hilo.

“Kazi iliyo mbele yetu ni ya ushindi na haina mbadala na hilo, na hii
ni Serikali ya CCM na wote waliochaguliwa na rais wanatumikia CCM na
wanatakiwa wakiheshimu kwani hata hawa mawaziri watatu wa vyama
pinzani niliowachaguwa wanaimani na CCM,” amesema.

Aidha Dkt. Shein alifahamisha kwamba hawatotumia mapanga wala vitisho katika kuiongoza nchi bali watatumia katiba na kanuni.







About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search