DARUSO: Vijana acheni kulalamika...soma habari kamili na matukio360..#share

Na Salha Mohamed,Dar es Salaam 

VIJANA nchini wametakiwa kufuatilia fedha zinazotolewa kwa kila halmashauri  ili kutumia  fursa  hiyo  kubuni miradi mbalimbali na kujikwamua kiuchumi. 
Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu Dar es Salaam (DARUSO), Jeremiah Jilili (wapili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mchango wa vijana kuelekea nchi ya viwanda na uchumi wa kati leo jijini Dar es Salaam. 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na rais wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO), Jeremiah Jilili wakati akitoa dira ya nchi na mchango wa vijana kuelekea nchi ya viwanda na uchumi wa kati.

Amesema vijana wanapaswa kuacha kulalamika mitaani na vichochoroni na badala yake wafanye utafiti na kuwasilisha mambo serikalini kwa maslahi ya nchi. 

"Tunapaswa kuishauri halmashauri kuanzisha miradi itakayokuwa chini ya vijana kama njia pekee ya kupunguza tatizo la ajira kwani halmashauri inayo nafasi kubwa ya kusaidia kuinua uchumi wa vijana walioanzisha miradi yao kwa miezi sita ya mwanzo,"amesema. 

Amesema serikali inahitaji mawazo ya vijana ili kutatua changamoto na si kulalamika pekee hivyo wathamini, wajali na kuhimiza utalii wa ndani ili kuongeza pato la taifa.

Amesema ili kufanikisha serikali ya viwanda, serikali inapaswa kuwekeza katika Kilimo cha kisasa kitakachohakikisha upatikanaji wa malighafi ya kutosha.

"Vijana inabidi tuwe mstari wa mbele kushiriki kwenye Kilimo kwani tutajihakikishia malighafi katika viwanda vyetu pamoja na chakula, "amesema. 

Amesema jambo hilo litaboresha na kuongeza shule zitakazofundisha masomo ya kilimo kwani somo hilo limekuwa si muhimu hasa katika shule zilizo ukanda wa Kilimo.

Amesema vijana wamekosa uzalendo dhidi ya taifa lao na kuwa waumini dhidi ya makundi kuliko taifa. 

"Si kitu kizuri kwa kijana kuwa mfia dini, chama na ukabila hadi kufikia hatua ya kujenga uadui kisa utofauti si hekima, busara kwa kijana mzalendo, "amesema. 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje DARUSO, Malisa Martine amesema serikali inapaswa kupunguza kodi kwa vijana wanaotaka kuanzisha miradi ili waweze kujiajiri. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search