Makamo wa rais Zanzibar 'awalilia' wafanyabiashara...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MAKAMO wa pili wa rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika kwa wafanyabiashara wakubwa
Zanzibar kuwekeza katika bidhaa za kiswahili hususan katika uchapishaji wa
vitabu vya kiswahili pamoja na kujenga maduka makubwa ya kuuzia bidhaa hizo.
Ametoa wito huo leo katika
ufungaji wa kongamano la kiswahili lililofanyika ukumbi wa zamani wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar.
Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko
la utungaji wa vitabu vya kiswahili na usomaji.
Amesema pamoja na kuwa Zanzibar ina watunzi wengi wa
vitabu vya kiswahili lakini imekuwa tabu kuvipata vitabu kutokana na kuwa hakuna utaratibu mzuri wa upatikanaji wake.
“Kiswahili ni bidhaa
inayouzika, wakati umewadia kwa wafanyabiashara wetu wakubwa kuwekeza katika
bidhaa hii katika uchapishaji wa vitabu vya kiswhaili, leo hii hapa Zanzibar
ukitaka vitabu vya waandishi wetu mashuhuri kama Profesa Said Ahmed , Shafi
Adam Shafi, Bwana Musa na ndugu yangu Mohammed Seif Khatib huvipati”, amesema
Balozi Seif.
Makamo huyo wa rais amesema
ni wakati muafaka sasa kufikiria kuandaa maonesho ya kimtaiafa ya vitabu vya kiswahili
katika ukanda wa Afrika Mashariki yatakayokuwa kila baada ya miaka miwili au
zaidi.
Amesema maonesho hayo pia
yatasaidia kuongeza kasi ya uchapishaji na usomaji vitabu.




No comments:
Post a Comment