Kesi ya Aveva, Kaburu DPP arejesha jalada Takukuru..soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu,Dar es
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amerejesha TAKUKURU Jalada la uchunguzi la kesi ya utakatishaji wa fedha wa USD 300,000, inayowakabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake,Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu na kuelekeza uchunguzi zaidi ufanyike.
Hayo yamesemwa leo na Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.
Swai alidai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika.
Pia alidai kuwa jalada la kesi hiyo lililokuwepo kwa DPP limekwisha rejeshwa na ameelekeza uchunguzi zaidi ufanyike na kwamba uchunguzi huo umekwishaanza kuwa ajili ya kukamilisha maeneo ambayo DPP ameelekeza.
Swai pia aliieleza mahakama kuwa wanaomba ufunguo kutoka kuwa mshtakiwa wa kwanza Aveva ili waweze kupata nyaraka ikiwa sehemu ya kukamilisha upelelezi.
Alibainisha kuwa Aveva alikuwa na ofisi mbili ya Simba na binafsi na kwamba katika ofisi hiyo binafsi kuna nyaraka za Simba.
Hivyo walimuandikia barua kupitia gerezani ili aweze kuruhusu upatikanaji wa funguo ili waweze kupata nyaraka zinazohitajika lakini hawajajibiwa. Swai aliomba upande wa utetezi uharakishe wapate hizo nyaraka ili waweze kukamilisha upelelezi.
Wakili wa utetezi, Evodius Mtawala aliieleza mahakama kuwa Aveva ameipata barua hiyo na kwamba juhudi zinaendelea kufanyika na nyaraka zilizoombwa zinaendelea kukusanywa na zitawasilishwa hivi karibuni.
Baada ya kutolewa maelezo hayo,Hakimu Nongwa aliiahirisha kesi ndani ya siku 14 ili pande hizo zote zikamilishe taratibu hizo, kesi imeahirishwa hadi Desemba 28,2017.
Evans Elieza Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.
Washtakiwa wapo rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili halina dhamana.
Katika kesi inayowakabili vigogo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) akiwamo, Jamal Malinzi imeahirishwa hadi Desemba 28,2017.
Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba ameagiza upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka.
Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga.
Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashitaka 28, yakiwamo ya utakatishaji fedha wa Dola za Marekani, 375,418.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment