LHRC: Nchi inapita katika hali ngumu...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abraham Ntambara
KITUO cha sheria na haki za binadamu (LHRC), kimesema nchi
kwa sasa inakabiliwa na hali mbaya kwenye haki za kisiasa, kiraia na uhuru wa
vyombo vya habari kuliko kipindo
chochote kuwahi kutokea nchini.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Dk Hellen Kijo Bisimba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Hellen Kijo Bisimba ameeleza
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe za kuadhimisha siku ya
kimataifa ya haki za binadamu inayoanzimishwa kila Desemba 10 na kwamba wameazimisha jana ili kuipisha serikali itakayoadhimisha Desemba 10 .
“Kama nchi tunamatatizo makubwa kwenye haki za kisiasa,
kiraia na uhuru wa vyombo vya habari,” amesema Dk. Kijo Bisimba.
Ametaja haki hizo nkuwa kutokuwapo kwa mikusanyiko ya kisiasa, maandamano,
kujieleza na uhuru wa kupata habari na kuripoti kwa upande wa vyombo vya
habari.
“Juzi juzi tulikuwa na mkutano na waandishi wa habari
tulivyomaliza tu vyombo vilivyotoa taarifa vikaitwa na mamlaka ya mawasaliano
nchini (TCRA) kwa ajli ya kujieleza kwa nini wametoa zile habari,” ameeleza.
Hata hivyo ameipongeza serikali katika kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma na kwamba vimeanza kupungua.
Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kujitathimini na nini kifanyike kuhakikisha haki za binadamu
zinaendelea kulindwa na kuheshimiwa.
"Baada ya majadiliano, tutapelekea mapendekezo yetu kwa lengo la kuishauri serikali nini chakufanya ili nchi iendelee kuwa salama katika kipindi cha mpito cha mkakati wa kuelekea uchumi wa viwanda vya kati,'' amesema.
No comments:
Post a Comment