Prisons kuongeza wachezaji watatu...soma habari kamili na matukio360...#share

Yusta Nkwelengushe, Mbeya
UONGOZI wa Tanzania Prisons umesema katika kipindi
hiki cha usajili wa dirisha dogo utaongeza wachezaji watatu na hautaacha mchezaji hata mmoja.
Timu ya soka ya Prisons
Prisons yenye kikosi cha wachezaji zaidi ya 25
inaendelea na mazoezi katika uwanja wake wa Magereza kwa ajili ya kuhakikisha
inaendeleza rekodi ya kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu Bara
inayotarajia kuendelea wiki ijayo.
Katibu wa klabu hiyo, Havintish Abdallah amesema nafasi hizo ni kiungo, golikipa na nafasi
nyingine moja ya ziada ili kuwa na wachezaji wa kutosha .
Amesema kwa sasa hawezi kuweka wazi majina na timu
wanazotoka wachezaji hao kutokana na kukwepa ‘figisu’ za kuchukuliwa na timu
nyingine.
Taarifa za uhakika ambazo mwandishi amezipata ni
kwamba uongozi wa maafande hao umepenya
jicho lake Zanzibar walikoweka kambi kabla ya kuanza kwa pazia la ligi msimu
huu.
Abdallah amesema “Tupo katika mchakato huo na
mazungumzo yetu na wachezaji tunaowahitaji
yanakwenda vizuri na muda wowote tunawasainisha kandarasi ya kuungana na
wenzao katika kulisukuma gurudumu hili’’.
Amesema ingawa wana kikosi cha wachezaji zaidi ya 25
lakini wameona ni vyema wakaongeza nafasi hizo tatu kutokana na ugumu wa ligi
unavyoonekana.
‘’Ligi ni ngumu kwa hiyo kipindi hiki tunatumia
kuboresha kikosi ili tuweze kupambana kikamilifu na kuweza kumaliza ligi katika
nafasi nzuri,’’amesema Abdallah
Tanzania Prisons inashika nafasi ya sita kimsimamo
kati ya timu 16 zinazoshiriki ligi ikiwa imevuna pointi 15 baada ya kucheza
mechi 11 ikiwa imefungwa mechi
mbili,kutoa sare sita pamoja na kushinda mechi tatu.
No comments:
Post a Comment