Lukuvi kukutana na wataalam wa ardhi...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Heri Shaaban, Dar es salaam
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa mwaka wa wataalam wa ardhi waliosoma chuo cha ardhi Morogoro .
I
Waziri wa ardhi, William Lukuvi
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa wataalam waliosoma chuo cha ardhi Morogoro, Salum Shaka amesema mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwezi Machi, 2018 ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya umoja huo inayofanyika kila mwaka.
"Umoja wa wataalam waliosoma chuo cha ardhi Morogoro tumeweka utaratibu kila mwaka tunafanya tathimini na kujadili maendeleo ya umoja wetu," amesema Shaka
Amewataka wataalam wote ambao wamesoma chuo hicho wajitokeze kuzungumza na waziri katika viwanja vya chuo hicho.
" Siku hii ni maalum kwetu ambapo mwanzoni mwa machi 2018 tutakutana mambo mbalimbali ya chuo yatajadiliwa kwa lengo la kupanua wigo wataalam kwa wataalam kujenga uwezo katika utendaji wa majukumu yetu na kujenga weledi wakiwa kazini," amesema.
Amesema siku hiyo ni maalum kwa kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya ardhi.
Amesema kwa sasa nchi inaelekea kwenye uchumi wa kati na kauli mbiu siku hiyo ni "Ardhi ni msingi mkuu kufikia azma ya Tanzania ya Viwanda."
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment