Mwenyekiti CCM apata ajali na familia yake...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi weti, Singida
MWENYEKITI wa CCM mkoa wa Singida Juma Kilimba ,mkewe na watoto wao watatu wamejeruhiwa baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka eneo la Msigiri wilayani Iramba mkoani Singida.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Juma Kilimba
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Jamson Mhagama amesema ajali hiyo ilitokea mchana na Kilimba alilazwa katika Hospitali ya Kiomboi huku mkewe Kilimba na wanawe walipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Itigi na kuwa CCM mkoani Singida inaendelea kusimamia matibabu yao.
Amesema mmoja kati ya watoto hao anapatiwa huduma katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment