Madabida wenzake wapata dhamana....soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefanikiwa kupata dhamana  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Ni baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuwasilisha cheti kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo kimeipa mamlaka mahakama hiyo ya Kisutu kuisikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo washtakiwa hao walisomewa mashtaka mapya matano mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa.

Katika mashtaka hayo mawili ni ya kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya Ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa kutendeka na kusababisha hasara. 

Ambapo shtaka lililokuwa likiwakabili awali la kula njama limeondolewa kwenye hati hiyo ya mashtaka.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na wapo nje Kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaominika ambapo kila mdhamini asaini bondi ya Sh 12 milioni.

Pia washtakiwa hao watoe fedha taslimu Sh 12 milioni ama mali isiyo hamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Hata hivyo washtakiwa hao wanikiwa Kwa kuwasilisha hati za Mali zilizohamishika. Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na washtakiwa watasomewa maelezo ya awali Januari 17,2018.

Katika kesi hiyo mpya washtakiwa wanaokabiliwa ni Madabida  ambaye ni afisa mtendaji mkuu, Seif Shamte ambaye ni mkurugenzi  wa uendeshaji,  Simon Msoffe meneja masoko na  Fatma Shango mhasibu msaidizi wote wa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd. Pamoja na Sadick Materu na Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa.  


Kimaro alidai kuwa  washtakiwa Madabida,  Seif, Simon na  Fatma Aprili 5, 2011 jijini Dar es Salaam waliisambazia Bohari Kuu makopo 7776 ya  dawa bandia za ARV’s zenye mchanganyiko wa dawa ya stavudin 30mg +nevirapine 200mg+lamivudine 150mg.

Dawa hizo zilizotengezwa Machi 2011 na kuisha muda wake wa matumizi Februari 2013 zilionyesha kuwa ni halali wakati si kweli.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuisambazia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kopo 4476 .

Washtakiwa hao wanadaiwa kujipatia Dola za Marekani 98,506.08  ambazo ni sawa na Sh 148,350,156 za Tanzania kwa udanganyifu baada ya kuonyesha kwamba fedha hizo ni malipo ya makopo 12252 ya dawa hizo za ARV’s.

Washtakiwa  Sadick Materu na Evans Mwemezi  wanadaiwa kuwa  kati ya Aprili 5 na 13 mwaka 2011 wakiwa maafisa wa Bohari Kuu ya Dawa walishindwa kuzuia kosa kutendekea.

Washtakiwa  hao wote, wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kutimiza wajibu na kuisababishia MSD  hasara ya Sh 148,350,156.48 kwa kusambaza dawa hizo bandia za kufubaza makali ya Ukimwi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao walikana.

Mwisho


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search