Uamuzi kesi vigogo wa MSD Januari...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu,Dar es salaam
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Januari 29,2018 inatarajia kutoa uamuzi iwapo vigogo wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wanaokabiliwa kesi ya vipimo feki vya kupimia Ukimwi kama wana kesi ya kujibu ama la.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Januari 29,2018 inatarajia kutoa uamuzi iwapo vigogo wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wanaokabiliwa kesi ya vipimo feki vya kupimia Ukimwi kama wana kesi ya kujibu ama la.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa siku hiyo na Hakimu Mkazi Mwandamizi,VictoriaNongwa.
Ni baada ya Mashahidi watatu wa upande wa mashtaka kutoka ushahidi wao na kuufunga.
Upande wa mashtaka katika kesi hiyo unawakilishwa na wakili wa Takukuru, Vitalis Peter huku utetezi ukiwakilishwa na wakili Makali Masatu.
Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Oparesheni Kanda ya Kaskazini wa MSD, Sylivester Matandiko , Naibu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, ambaye pia ni Meneja wa Viwango, Sadiki Materu na Wasajili kutoka Bodi ya Maabara Binafsi ya Afya Zainabu Mfaume na Joseph Nchimbi.
Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka saba ya kutumia madaraka vibaya na kuisabishia hasara serikali ya zaidi ya Sh 3bilioni kwa kuruhusu uingizaji wa vipimo feki vya kupimia HIV.
Kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 20 na Julai 20, 2012, walikula njama ya kutenda makosa hayo na kutumia madaraka yao vibaya kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment