Makalla atengua maamuzi ya mkuu wa wilaya....soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Mbarali
MKUU wa mkoa wa Mbeya, Amos
Makalla ametengua agizo la mkuu wa wilaya ya mbarali na kuagiza wakulima
waendelee kulima mazao yao hususan mpunga kwa kutumia skimu ya umwagiliaji maji.
Mkuu wa Mkoa Amos Makalla(katikati) akiangalia namna uharibifu wa mazingira uliofanywa kwenye kingo za mto Mbarali kutokana na shughuli za kilimo cha umwagiliaji kusho) kwake ni mkuu wa wilaya hiyo, Reumen Mfune.
Hivi karibuni mkuu wa wilaya
ya Mbarali, Reuben Mfune aliagiza kufungwa kwa skimu ya umwagiliaji ya mnazi
iliyopo katika kata ya Imalilo Usongwe kwa madai ya kuharibu vyanzo vya maji
vya mto ruaha.
Lakini jana katika mkutano
wake wa hadhara uliofanyika katika kata ya Imalilo Usongwe, Makalla ameagiza kuchimbwa mfereji wa skimu uliokuwa
umefukiwa na kwamba serikali wilayani humo ndio iliyoshindwa kuhusimamia na
kuweka sawa miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima.
Amesema licha ya
wakulima kutumia mfereji huo bila kibali,changamoto iko kwa
serikali kwa kuwa haikuandaa mipango ya kuboresha miundombinu ya kilimo cha
umwagiliaji .
Makalla amesema kitendo
cha kufunga mfereji kunaweza kusababisha zaidi ya hekari 5,700 kutolimwa katika msimu huu wa kilimo na
takribani wakulima 2,000 wanaweza
kukosa chakula suala ambalo ni hatari kwa taifa.
"Kuanzia leo(jana) kaendeleeni na shughuli za kilimo pia
toeni ushirikiano kwa
viongozi wa halmashauri kufukua mfereji
na sipendi kusikia kuna tofauti au kuwepo kwa vitendo vya kuwakwaza wananchi katika zoezi hilo,"alisema
Makalla.
Amesema uchumi wa viwanda hauwezi kufanikiwa kama
wakulima watakosa sehemu ya kuzalisha mazao kwa sababu ya ukosefu wa maji.
“Kimsingi kosa lilifanywa na Serikali kwa kutoandaa
mazingira rafiki na ndio tumefikia hatua
hii,’’ amesema.
Awali mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune, alieleza sababu ya kufungwa kwa
skimu hiyo ni kutekeleza agizo
lililotolewa na kikosi kazi kilichondwa na makamu wa rais, Samia Suluhu
kutokana uharibifu unaofanywa katika
hifadhi ya mto ruaha kunakosababishwa na shughuli za kilimo cha umwagiliaji .
Mbunge wa jimbo la Mbarali (CCM) Haroon Mulla,
alipongeza maamuzi ya mkuu wa mkoa huyo
wa kwamba amekuwa akichukiwa na wananchi wake kutokana na chokochoko za
kisiasa.
"Wananchi
mnanichukia bure ninatambua kuna jinamizi limepita ambalo linanichonganisha
na nyinyi mimi nimepigania sana suala la
kufungwa kwa skimu hiyo kwa kutambua wananchi wangu mnajishughulisha
na kilimo ili kujipatia kipato,"alisema.
Mkulima, Christopher Bwagile alisema tangu mwaka 2001 waliomba
kibali cha kutumia mto mbarali kwa ajili ya kilimo cha umwagiliji lakini hadi
sasa hakuna majibu na ameiomba serikali
ya mkoa huo isimamie upatikanaji wa kibali ili watumie maji kihalali..



No comments:
Post a Comment