Mwanamke achomwa hadi kufa kwa 'kukataa' uchumba...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
MAAFISA wa polisi katika mji wa kusini mwa India wa
Hyderabad wamemkamata mwanamume, Karthika Vanga( 28) akituhumiwa kumchoma moto mwanamke Sandhya
Rani(25) hadi kufa kutokana na mgogoro
wa kimapenzi.
Alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja na bi Rani
hadi miezi michache iliyopita.
Wakati alipomkaribia siku ya
Alhamisi wawili hao walionekana wakijibizana kabla ya mwanamume huyo kuchukua
mafuta ya taa, na kumwagia mwilini na kumchoma moto , polisi walidai.
Walisema kuwa kulikuwa na
madai kwamba Vanga amekuwa akitaka kumchumbia bi Rani kwa kipindi cha miaka
miwili.
Alikuwa amekataa mara kadhaa
kuchumbiwa na bwana huyo ijapokuwa polisi wanasema haijulikani iwapo kulikuwa
na malalamishi dhidi ya mtu huyo.
Mashambulizi dhidi ya
wanawake nchini India yameongezeka tangu ubakaji wa gengi la mwaka 2012 na
mauaji ya mwanafunzi katika basi moja mjini Delhi, na yamesababisha kuwekwa kwa
sheria kali zinazolenga kukabiliana na mashambulio kama hayo.
Tayari nchi hiyo imeshapiga
marufuku talaka tatu na wanaume wanaotoa talaka tatu kwa mpigo hufungwa jela huku mabibi
harusi wanakabidhiwa silaha ya kujilinda India




No comments:
Post a Comment