Mfuko wa pamba wavunjwa...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu, Kassim
Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa kuendeleza zao la Pamba (CDTF) na amegiza
wahusika wote wachunguzwe ili kubaini fedha walizokusanya zimetumikaje.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Taarifa iliyotolewa
leo na ofisi ya waziri mkuu imesema, alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa
akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao alichokiitisha mkoani Shinyanga.
Lengo la kikao
hicho ilikuwa kufanya ufuatiliaji wa maagizo ambayo alikwishakuyatoa kwani alishafanya
vikao vitatu na wadau mbalimbali wa zao
hilo.
Alichukua uamuzi
huo baada ya kubaini kuwa watendaji wa mfuko huo hawajatekeleza majukumu ya
kuundwa kwa mfuko huo lakini pia majukumu yao yanaingiliana na yale ya Bodi ya
Pamba Tanzania (TCB).
“Kuna CDTF katika
zao la pamba lakini hakuna inachofanya ambacho kinawalenga wakulima moja kwa
moja. Tunaiondoa CDTF na kazi zake kuanzia sasa zifanywe na Bodi,” alisema.
“Waziri wa Kilimo
peleka timu ya ukaguzi kuona wamefanya nini hadi sasa. Tunataka Bodi ifanye
kazi na iulizwe maswali kuhusu zao hili. Endapo kuna jambo halijafanyika, Bodi
iwe na uwezo wa kutoa majibu si kusubiri tena mtu wa chombo kingine aje kutoa
majibu,” alisema Waziri Mkuu.
“Kwa muundo huu,
Mkurugenzi wa Bodi anakaa tu, wakati akisubiri kazi yake ifanywe na CDTF,”
aliongeza.
Mfuko wa CDTF
unaundwa na wajumbe sita ambao ni wawakilishi wa wakulima wawili, wawakilishi
wa wenye viwanda vya kuchambua pamba wawili, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba na
Mkurugenzi wa Mazao kutoka Wizara ya Kilimo.
Mfuko huu uliundwa
mwaka 1999 na Bodi ya Pamba (TCB) ili uwashirikishe wadau wa zao hilo kuondoa
matatizo yaliyojitokeza kwenye sekta hiyo baada ya Serikali kujitoa kwenye
uendeshaji wa moja kwa moja wa mazao nchini ikiwemo uzalishaji na biashara
kutokana na mfumo wa soko huria.
Desemba mwaka jana,
Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba alifikia uamuzi kama huo na kuamua
kusimamisha shughuli zilizokuwa zinafanywa na Mfuko wa Kuendesha Zao la Korosho
Nchini (CIDTF) ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za mfuko huo.




No comments:
Post a Comment