Ndege ituayo majini yaanza safari...soma habari kamili na matukio360..#share


Na mashirika ya kimataifa
NDEGE mpya kubwa zaidi duniani inayoweza kutua na kupaa kutoka majini ya China ya AG600, imefanya safari yake ya kwanza kwa jumla  ya saa moja.

Ndege ya China inayotua majini

Ndege hiyo ambayo ni kubwa kuweza kukaribiana na ndege ya Boeng ya 747 na yenye injini 4, ilipaa kutoka uwanja wa ndege wa Zhuhai katika mkoa ulio kusini wa Guangdong.

Ndege hiyo inaweza kubeba watu 50 na kusalia hewani kwa saa 12. Ina mitambo ya kuzima moto na inaweza kufanya shughuli na uokoaji baharini na pia inaweza kutumwa kwenda eneo linalozozaniwa kusini mwa habari ya China.

Vyombo vya habari nchini China viliitaja ndege hiyo kama mlinzi wa bahari na visiwa. Imechukua miaka minane kuunda ndege hiyo iliyo na uzito wa tani 53.3.
Kupaa kwa ndege hiyo kulitangazwa moja kwa moja katika runinga ya taifa na ililakiwa na umati wa watu waliopeperusha bendera wakati ikitua.


Tayari kuna kandarasi 17 za kujenga ndege hiyo kutoka ndani ya China. Sera ya China ya kusini mwa bahari mwa China inapingwa vikali na nchi kadhaa majirani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search