MO Dewji amtaka Omog aachie ngazi Simba...soma habari kamili na matukio360..#share


Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
KATIKA hali ya sintofahamu bilionea Mohammed Dewji amemtaka kocha  mkuu wa timu ya Simba, Mcameroon Joseph  Omog ajiuzulu.

Mohammed Dewji

Bila kutaja sababu Dewji jioni ya leo majira ya saa kumi  Desemba 23/12/2017 katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook ameandika ; "Kwa kuwa bado sina mamlaka ya maamuzi kwenye klabu ya simba, kama mwanachama na shabiki wa simba, namuomba Omog kwa heshima na taadhima ajiuzulu.’’

Mo ambaye ni mfanyabiashara  anatoa kauli hiyo ikiwa ni miezi michache kushinda dhabuni ya kuwa mwekezaji katika klabu ya Simba.

Mo Dewji alishinda zabuni ya kuwa mwekezaji wa Simba kwa dau la Sh bilioni 20 alizoweka ‘mezani’ ambapo Simba sasa inamilikiwa na pande mbili, wanachama na Mohamed Dewji.

Kufuatiwa na kuwa mmilikia halali wa timu hiyo, Dewji ametoa ahadi kumi kwa klabu hiyo ya Simba.

1. Kambi ya Simba itajengwa upya kabisa na itakuwa ni hosteli ya kisasa yenye vyumba hadi 35. 30 vitakuwa kwa ajili ya wachezaji na vitano kwa ajili ya benchi la ufundi.

2.Simba sasa itafaidika kwa kuwa na gym yake ya kisasa, bwawa kubwa la kuogelea kwa ajili ya mazoezi na sehemu ya kupumzika kwa wachezaji.

3.Wachezaji, makocha na viongozi watakuwa na mgahawa wao wa kisasa kabisa.

4. Mo Dewji anaamini timu lazima iwe na viwanja vya mazoezi. Hivyo ataanza na viwanja viwili, kimoja nyasi asilia na kingine nyasi bandia.

5. Mo Dewji ameahidi kuwekeza katika soka la vijana akianza na wale wenye umri wa chini ya miaka 14, 16 na 18 na lengo ni kuwakuza.

6. Mo Dewji amesema atasimamia wachezaji kuitambua thamani ya Simba kwa kujituma hasa.

7. Simba itaanza kufanya mambo kimataifa kwa kuitangaza na kuikuza brand ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa mbalimbali kama fulana, kofia, vishika ufunguo na kadhalika.

8. Ameahidi kutenga kitita cha  Sh milioni 500 ambazo zitatumiwa na benchi la ufundi katika mipango yao kama kambi na kadhalika pia Sh bilioni moja kwa ajili ya usajili.

9. Kushindana na timu kubwa Afrika na sio Tanzania pekee.


10. Kurejesha Simba katika historia ya kimataifa

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search