Ngono yamfukuzisha kazi naibu waziri mkuu...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa

NAIBU wa waziri mkuu wa Uingereza, Damian Green, ameachishwa kazi baada ya kubainika kuwa alikiuka kanuni za uwaziri.
Damian Green

Green ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Waziri mkuu Theresa May alibainika kuwa alitoa taarifa zisizo sahihi kuhusu picha za ngono zilizokutwa kwenye kompyuta yake ya ofisini.

Pia Damian Green alikuwa anachunguzwa juu ya madai ya kutowaheshimu wanawake wanaharakati katika chama chake cha Conservative.

Hata hivyo kiongozi huyo amekanusha kuhusika na mashitaka yote yanaomkabili.


Wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema kuondoka kwa kiongozi huyo ni pigo kubwa kwa waziri mkuu .

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search