Vigogo wanne NHC warejeshwa kazini...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

WAKURUGENZI wanne kati ya watano wa shirika la nyumba la taifa(NHC) waliosimamishwa kazi mapema wiki, wamerejeshwa tena kazini, matukio360 inakuthibitishia hilo.


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Uamuzi huo wa kuwarejesha umefikiwa jana na wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waliorejeshwa ni mkurugenzi ubunifu, Issack Peter, mkurugenzi wa rasilimali watu,James Rhombo, mkurugenzi fedha na maendeleo ya biashara, David Shambwe na mkurugenzi wa usimamizi wa milki, Hamad Abdallah.

Duru huru za habari kutoka wizarani humo zimeeleza kuwa uamuzi wa kumrejesha mkurugenzi wa utawala na huduma za mikoa, Raymond Mdolwa bado haujafikiwa kwa sababu kadhaa.

"Siwezi kukutajia sababu za Mdolwa kutorejeshwa kazini lakini hawa wanne wote wamerejeshwa kazini na leo hii (Alhamisi Desemba 21/12/2017) wapo ofisini wakiendelea na majukumu yao kama kawaida. Huu ni uamuzi uliofikiwa na wizara ya ardhi,’’ kimesema chanzo chetu cha kuaminika kutoka wizarani humo.

Uchunguzi uliofanywa na matukio360 umebaini mapema wakurugenzi hao wote wamefika kazini makao makuu ya NHC upanga jijini Dar es Salaam, kuendelea na majuku yao.

Mapema mwanzoni mwa wiki hii kikao cha bodi ya Wakurugenzi chini ya mwenyekiti wake, Blandina Nyoni kilifanya kilitoa maamuzi ya kusimamishwa kazi kwa wakurungezi hao ikiwa ni siku chache aliyekuwa mkurugenzi wa shirika hilo,Nehemia Mchechu kusimamishwa kazi

Mbali na hao, pia ilidaiwa wafanyakazi wote wa ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC na wahudumu nao wamesimamishwa.

Pia bodi hiyo ya wakurugenzi wa shirika hilo, imemteua Felix Maagi kuwa Kaimu Mkurugenzi wa NHC.

Kusimamishwa kazi kwa Mchechu kulitangazwa na idara ya habari maelezo ikunukuu agizo la waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search