Serikali kuipa ushirikiano Dubai....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema
itahakikisha inatoa ushirikiano kwa Shirika la Ndege la Dubai (Fly Dubai), ili lifanye
kazi zake vizuri za utoaji wa huduma za usafiri wa anga hapa nchini.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Anna Mgwira (kulia), Makamu wa Rais Uendeshaji Biashara wa Shirika
la Ndege la FlyDubai, Sudhir Sreedharan (wa pili kushoto), wakikata keki
kuashiria uzinduzi rasmi wa safari za Ndege za Shirika hilo katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza leo mkoani
Kilimanjaro katika uzinduzi wa safari za ndege kutoka Uwanja wa ndege wa
Kilimanjaro (KIA) kuelekea nchini Dubai, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema uzinduzi wa safari hizo utakuza
sekta ya utalii na biashara mkoani humo na nchi kwa ujumla.
"Naamini kupitia
uzinduzi huu uchumi wetu utakua kwani wafanyabiashara na watalii kutoka nchi
mbalimbali wataweza kuongezeka zaidi sababu wamesogezewa huduma za usafiri wa
ndege za kimataifa katika viwanja vya ndege vikubwa nchini", amesema
Waziri Prof. Mbarawa.
Profesa Mbarawa
ameuhakikishia uongozi wa shirika hilo la ndege kuwa hawatojutia uamuzi wao wa
kuamua kusogeza huduma zao za usafiri katika uwanja huo kwani wafanyabiashara
wengi na wananchi kutoka sehemu mbalimbali wamekuwa wakitumia uwanja huo.
Kwa upande wake Makamu
wa Rais wa Shirika la ndege la Dubai, Sudhir Sreedharan, amesema kutokana na umuhimu na ubora wa uwanja huo
wameamua kusogeza huduma zao kutokana na kuamini kuwa wageni wengi wa kimataifa
wamekuwa wakitumia uwanja huo kwenda sehemu mbalimbali za vivutio vya utalii
mkoani humo na mikoa ya jirani ya Arusha na Manyara.
"Kuna mambo mengi yametuvutia kuanzisha safari zetu katika uwanja huu, tunaamini hata soko letu la biashara litafanikiwa kwa kuongeza huduma hapa", amefafanua Makamu wa Rais.
"Kuna mambo mengi yametuvutia kuanzisha safari zetu katika uwanja huu, tunaamini hata soko letu la biashara litafanikiwa kwa kuongeza huduma hapa", amefafanua Makamu wa Rais.
Shirika la ndege la
Dubai, sasa litatoa huduma za usafiri wa anga katika viwanja vya ndege vitatu
kikiwemo kilichozinduliwa leo cha KIA na vile viwanja viwili vya ndege vya
Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) na Uwanja wa ndege wa Zanzibar vilivyokuwa awali.
No comments:
Post a Comment