Timu ya serikali Mbeya kujipima na Azam veterani...soma habari kamili na matukio360..#share


Yusta Nkwelengushe, Mbeya
Timu ya viongozi wa Serikali kutoka Mkoa wa Mbeya inatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki na Maveterani wa mkoa  wa Dar es salaam na Morogoro.

Timu ya soka ya serikali mkoani Mbeya. Watatu kutoka kulia waliosimama ni mkuu wa mkoa huo,Amos Makalla

Tayari kikosi cha wachezaji 20 cha Timu ya viongozi wa Serikali  kutoka Mkoa wa Mbeya kiliondoka jana mkoani hapa kikiwa na matarajio ya kushinda.

Kocha mchezaji wa timu ya viongozi wa serikali ,Amos Makalla amesema mechi ya kwanza wanatarajia kucheza kesho (Jumamosi) na Azam Veteran kwenye Uwanja wa Chamanzi jijini Dar es salaam.

Amesema " Leo tunatarajia  kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam , ni imani yetu kwamba tutaibuka na ushindi mnono'.

Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa huu amesema  baada ya kucheza mechi ya Jumamosi wataondoka hadi mkoani Morogoro  kucheza na Maveteran wa Mkoa wa Morogoro siku ya Jumapili.

"Tunaushukuru Uongozi wa Azam kutualika kucheza mechi hii,hii inaleta uhusiano mzuri baina ya mkoa na mkoa na pia michezo ni sehemu ya kuimarisha afya kwa wafanyakazi," amesema Makalla.

A mesema uanzishwaji wa timu hiyo umeifanya jamii kuhamasika kupima Virusi vya Ukimwi pamoja na kusafisha mazingira.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search