Wachezaji Zanzibar Heroes wapewa viwanja, milioni tatu...soma habari kamili na matukio360..#share


Na Mwajuma Kombo, Unguja
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amewatunuku  wachezaji 33 wa timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ kiwanja na shilingi milioni tatu kila mmoja kufuatia kushika nafasi ya pili katika  michuano ya Chalenji iliyofanyika nchini Kenya Disemba 2017.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakati wa hafla ya chakula maalum alichowaandalia na kuwakabidhi zawadi.(Picha na Ikulu)

Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo ilifanyika usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni mjini Unguja na kuambatana na taarab asilia  iliyotumbuizwa na Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar.

Viwanja hivyo walivyopewa wachezaji hao wametakiwa kuvitumia wao wenyewe kwa ujenzi wa makazi na si kuviuza.

Akizungumza katika hafla hiyo Dk. Shein alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki yenye historia  katika  mpira wa miguu na hatua waliyofikia wamedhihirisha hilo.

“Pamoja na kwamba nimetoa zawadi hizi lakini bado zijaridhika sana, nilidhamiria niwapongeze kuliko hivi, dhamira yetu ilikuwa si ya kushiriki ni ya kushinda na Zanzibar ilishinda”, alisema Dk. Shein.

Ameahidi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kuwekeza na kuiendeleza timu hiyo ili kuwa bora zaidi.

“Tutatafuta njia muhimu na walimu wetu tutawaongezea nguvu ,
Zanzibar ina historia ya kuwa na walimu wazuri wa soka,” alisema.

Pamoja na mambo mengine ameiagiza wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kuongeza kasi  katika michezo  hasa kuandaa mipango kabambe ya mpira.

Aidha alikitaka chama cha soka Zanzibar (ZFA) kuacha  kwenda mahakamani na kama mtu hawezi kuongoza atoke ndani ya chama hicho kwani tabia ya kwenda mahakamani wanaiondolea heshima Zanzibar katika soka.


Zanzibar ilishiriki michuano ya Chalenji inayoandaliwa na CECAFA ambapo ilipata nafasi ya pili  baada ya kufungwa na Kenya ambao ndio walikuwa wenyeji wa michuano hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penanti 3-2.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search