Waratibu elimu wawili washushwa vyeo...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Kongwa
WARATIBU elimu kata wawili
wa kata za Njoge na Lenjulu wilayani Kongwa mkoani Dodoma wameshuswa vyeo kwa
makosa ya ulevi na kutokuwajibika katika masuala ya maendeleo mashuleni.
Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Deogratias Ndejembi
Agizo la kushushwa vyeo kwa
waratibu hao lilitolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratias Ndejembi
wakati akizungumza na waratibu elimu kata 22 katika kikao cha mapokeo ya kidato
cha kwanza na darasa la kwanza mwaka 2018.
Waratibu waliosimamishwa ni
Emmanuel Chiluluse wa Kata ya Lenjulu na Venance Mwangasa wa Njoge.
"Hawa watu hawatambui
kazi zao hivyo naagiza afisa elimu msingi na sekondari muwatafutie kazi
nyingine za kufanya na mtafute watu wengine wa kuziba nafasi zao" alisema
Ndejembi.
Ndejembi alisema waratibu wa
namna hii hawafai katika wilaya yake kwani wanachochea kushuka kwa kiwango cha
elimu na kukiuka ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) chini ya mwenyekiti wake
Rais John Magufuli,"alisema Ndejembi
Mkuu wa wilaya aliwataka
waratibu elimu kata kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wabadirike na
kuendana na kasi ya serikaki ya sasa.
Ofisa elimu sekondari wilaya
Kongwa Nelson Milanzi alisema waratibu wengi wanajichukulia wao ni waratibu wa
shule za msingi na sio sekondari jambo linalofanya msukumo na ufatiliaji wa
sekondari kushuka.
Kuhusu ufaulu kwa wanafunzi
Milanzi alisema wanafunzi 3863 wamepangwa kuripoti kidato cha kwanza katika
shule za sekondari 26 wilayani Kongwa na tayari wakuu wa shule wamepatiwa
majina ya wanafunzi hao.
Mwenyekiti wa kamati za
kudumu za jamii na diwani wa kata ya Sejeli Chilingo Chimeledya alisema kuna
upungufu wa madarasa 20 katika shule zote za sekondari hivyo amewataka viongozi
wa kata kushirikiana na wananchi kutatua changamoto hiyo.
Diwani huyo aliwataka
viongozi wa kata na wanasiasa kusaidiana na kushirikiana katika kuhamasisha
upanuzi wa miundombinu na ujenzi wa madarasa.
Chilingo pia alizungumzia
suala la mazingira akiwaomba viongozi wa shule za sekondari Norini, Sagara na
Mlali zinazootesha miti kuendelea kugawa katika shule nyingine katika kuboresha
mazingira na kutekeleza agizo la makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.




No comments:
Post a Comment