Wajue nguruwe wenye sura mbaya zaidi Duniani...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
WANASAYANSI wamepata picha za kwanza za msituni za nguruwe wachache wenye sura mbaya zaidi
duniani.
Mmoja wa nguruwe mwenye sura mbaya zaidi
Nguruwe hao kwa jina Javan
waty, wako kwenye hatari ya kuwindwa na kupotea katika makazi yao na wanasayansi
wanasema kuwa nguruwe hao tayari wanaelekea kuangamia.
Kamera fiche kwa sasa
zimefichua kuwa idadi ndogo ya nguruwe hao bado wanaishi maeneo ya misitu kadha
huko Java.
Wanasayansi wanasema kuwa
lengo lao ni kulinda makazi ya wanyama hao.
Mkuu wa utafiti huo Dk
Johanna Rode-Margono, alisema kuwa wanasayansi walifurahishwa kugundua kuwa
nguruwe hao bado wako.
Utafiti wa mwisho kwenye
misitu hiyo ulifanywa mwaka 2004 na kuonyesha kuwa idadi ya nguruwe hao ilikuwa
ikididimia zaidi.
"Tuliogopa kuwa wote au wengi zaid walikuwa
wametoweka."
Kati ya maeneo saba ambayo
wanasayansi waliyafanyia uchunguzi wakitumia kamera fiche, ni matatu tu
yaligunduliwa kuwa na nguruwe hao.
No comments:
Post a Comment