Kesi mhasibu wa Takukuru kuunguruma leo...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki
KESI inayomkabili
mhasibu  mkuu wa TAKUKURU,  Godfrey Gugai anayedaiwa kuwa na utajiri wa kutisha kwa kumiliki mali zenye
thamani ya sh. bilioni tatu ambazo haziendani na kipato chake, inaendelea leo  katika mahakama ya hakimu kazi Kisutu, jijini
Dar es Salaam.
Godfrey Gugai
Kabla ya leo, upelelezi wa
kesi hiyo ulikuwa bado haujakamilika.
Wakili wa Serikali Mkuu,
Vitalis Peter alidai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati
shauri hilo linalomkabili Gugai na wenzake watatu lilipopelekwa kwa kutajwa.
Hata hivyo, Wakili wa
utetezi, Alex Mgongolwa aliomba upande wa jamhuri watoe maelezo ambayo
yataeleza lini upelelezi utakamilika ambapo upande wao utajua siku ya kuanza
kwa usikilizwaji wa shauri hilo.
Wakili huyo alidai tarehe ya
leo wataeleza hatua ya upelelezi ilipofikiwa. 
Mbali na Gugai, washitakiwa
wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera.
Washitakiwa hao
wanaokabiliwa na mashitaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu,
kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya
viwanja katika maeneo mbalimbali.
Gugai na wenzake wanasota
mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashitaka ya utakatishaji fedha ambayo
hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
Katika mashitaka hayo,
shitaka la kwanza ni la kumiliki mali ambazo hazina maelezo ambalo linamkabili
Gugai  anayedaiwa kati ya Januari 2005 na
Desemba 2015, mkoa wa Dar es Salaam, akiwa ofisa wa umma ameajiriwa na TAKUKURU
anamiliki mali zenye thamani ya sh. 3,634,961,105.02 ambazo haziendani na
kipato chake cha sasa wala cha nyuma cha sh. 852,183,160.46 na alipotakiwa
kutoa maelezo alishindwa kuyatoa juu ya mali hizo zilizoko kwenye umiliki wake.




No comments:
Post a Comment