Magufuli: Wajanja walitaka kuchota bilioni 300.....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es
salaam
RAIS John Magufuli amesema watu wasiokuwa na nia njema
walitaka kuchota takriban sh  bilioni 300
kutoka katika mradi wa  mfumo wa uhamiaji
mtandao na hati ya kusafiria 'passport' ya kielektroniki.
Amesema vyombo vya usalama
ndivyo vilivyotumika kuokoa wizi huo  na amemtaka kamishna mkuu wa uhamiaji kuongeza
mbinu kudhibiti mianya mibovu katika idara hiyo.
Rais Magufuli amesema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua mradi huo na  kuwa awali
mapendekezo ya mradi huo ilikuwa ni sh bilioni 400 na  hadi unakamilika
umetumia sh bilioni 127.2
"Wajanja wachache wasiohitakia
mema Tanzania walikuwa wameshatengeneza dili la kuchota zaidi ya mabilioni
katika mradi huu, awali walisema ugegharimu sh bilioni 400 lakini kupitia
vyomba vya usalama nchini tukagundua kuna wizi unataka kufanyika.
"Tukafuatilia kwa makini
tukagundua mchezo huo, tukaudhibiti na sasa umegharimu sh bilioni127.2 tu. Ndio
maana hawa wapigaji walikuwa wakipita huku na huku kuweka vipingamizi kuhusu mrdi huu, walifikiri Tanzania bado ni ile ya zamani ya upigaji,’’ amesema   
Rais amesema idara ya uhamiaji
ni muhimu kwa usalama na uchumi wa nchini na kwamba bei ya hati mpya ya
kusafiria ya kielektroniki itagharimu sh 150,000 kwa miaka kumi ikiwa ni
wastani wa sh 15,000 kwa kila mwezi.
Amesema ongezeko la bei ya
hati ya kusafiria inatokana na ubora wake na ongezeko la kurasa nyingi kuliko ya zamani  na  imezingatia usalama
wa raia na nchi  
Amesema hivi karibuni idara
ya uhamiaji  ililega na kuwa uchochoro
kwa wahamiaji na wafanyabiashara hasa wafanyabiashara wa dawa za kulevya
ikiwamo kupewa  pasipoti mbili kinyume
cha sheria na raia wa kigeni kupata kibali cha ukaaji kiholela. 
Pamoja na mambo mengine
ameahidi kutoa milioni kumi za ujenzi wa ofisi mpya za makao makuu ya idara ya
uhamiaji.
Katika hatua nyingine rais
Magufuli ameagiza wahamiaji waliongia kinyume cha utaratibu kutafutwa na kukamatwa mahala
popote walipo.
"Ninataarifa kuwa
kuna wahamiaji 1500 wa kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
wameingia nchini lakini walioripoti ni chini ya 1000 sasa ninaagiza watafutwe
mahala popote walipo na hatua za kisheria zichukuliwe,’’ amesema
Amemtaka kamishna wa idara ya uhamiaji, Dk Anna Makakala
kuwachukulia hatua za kinidhamu watendaji na watumishi wa idara hiyo wanaokwenda
kinyume na utaratibu wa utendaji kazi.
“Jiulize  mhamiaji alifikaje katika mikoa mingine  hivyo wachukulie hatua za kinidhamu wakuu wa
uhamiaji wa mikoa waliyopita ikiwamo kuwashusha vyeo,’’ amesema
 Awali Waziri wa mambo ya
ndani, Dk Mwigulu Nchemba amesema mradi huo umezingatia mahitaji ya sasa na
kwamba wataanza kutoa hati za kusafiria za elekitroniki  kwa Afrika mashariki na vibali vyote kwa njia
ya mtandao.
Mradi huo umetengenezwa na
kampuni ya HDI grobu ya marekani 
kwa  uangalizi wa nchi ya  Ireland




No comments:
Post a Comment