Wanamitindo nchini waunda chama chao....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
WANAMITINDO nchini wameanzisha chama chao kinachoitwa FAT, kitachoshughulikia masuala mbalimbali ya wadau hao
Mwanzilishi wa FAT, Mustafa Hassanali akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chama cha wanamitindo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa chama cha wanamitindo Tanzania(FAT), Mustafa Hassanali amesema lengo la chama ni kuendeleza maslahi ya sekta ya mitindo kwa kuwaunganisha
na kugawana ujuzi, uzoefu na rasilimali katika sekta hiyo.
“FAT pia imelenga kukuza na kuimarisha sekta ya mitindo nchini. Sisi kama wabunifu
tunaunga mkono juhudi za rais Magufuli katika kuifanya nchi kuwa katika
uchumi wa viwanda vya kati ifikapo 2025 kwa kuongoza katika bidhaa za nguo na vitambaa
zinazotoka Tanzania,” amesema Hassanali.
Ameongeza “Sekta ya mitindo Tanzania inakuwa kwa haraka sana,
wadau wake wanakumbana na changamoto nyingi lakini bado tuna uhakika
wakati wa mafanikio umefika kupitia kuanzishwa kwa chama hiki chenye nia ya
kuimarisha uhusiano mzuri wa wafanyaji kazi za mitindo, wadau wa mitindo na nchini na Duniani kwa ujumla.”
Mmoja wa waanzilishi wa chama hicho, Asia
Idarous amesema chama hicho kimeundwa kwa ajili ya wadau wote wa sekta ya
mitindo na inajumuisha majukwaa mbali mbali kwa ajili ya mitindo, taasisi za
mitindo, wanamitindo wa kuonyesha mavazi (models).
Wengine ni wanamitindo wanaopanga muonekano wa mavazi
(stylist), wapiga picha wa mtindo, makampuni ya nguo, wazalishaji na wauzaji
mavazi na wanaojihusisha na kazi za mitindo na urembo.
Amewahimiza wafanyakazi katika sekta hiyo kujiunga
katika chama ili kupaza sauti zao kwa fursa mpya za mitindo, kutatua
changamoto za kazi za mitindo na kupanua mitandao yao.
No comments:
Post a Comment