Aliyemtunuku shahada ya uzamivu Grace Mugabe akamatwa Zimbabwe.... soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
NAIBU chansela wa chuo kikuu cha Zimbabwe, Levi Nyagura amekamatwa kuhusiana na utoaji wa wa cheti cha shahada ya uzamivu kwa mke wa rais wa zamani nchini humo Robert Mugabe.
Grace Mugabe
Grace Mugabe alitunukiwa cheti hicho baada ya kusoma kwa miezi michache na hoja yake ikachapishwa mwezi uliopita baada ya kuzuka kwa wito wa kupokonywa shahada hiyo
Tume ya uchaguzi inatarajiwa kumshtaki naibu huyo kwa utumizi mbaya wa ofisi.
Kile ambacho hakiko wazi ni iwapo bi Mugabe atakamatwa.
Badala ya kusoma miaka kadhaa alipokea shahada yake miezi kadhaa baada ya kusajiliwa katika chuo hicho.
Alikuwa akijaribu kuwa rais wa taifa hilo lakini baada ya jeshi kumuondoa madarakani Robert Mugabe mwezi Novemba mwaka jana harakati zake za kisiasa ziligonga mwamba hatua iliyowafurahisha raia wengi wa Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment