Tetesi Leo; Chelsea wamtega Costa # Man City watoa £60 kwa Sanchez # Arsenal wamtaka Asensio.. #share




http://fw-wordpress.s3.amazonaws.com/wp-content/uploads/2016/10/diego-costa-celebrates-goal.jpg

LONDON- MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu nchini (EPL), Chelsea, wanadaiwa kumpa masharti kadhaa ya kutimiza mshambuliaji wao anayetaka kuuzwa, Diego Costa (28) ili apate kuondoka klabuni hapo. Guardian.

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2015/02/06/255D56D500000578-2942492-Alexis_Sanchez_is_willing_to_defy_medical_advice_to_play_for_Ars-a-79_1423228483885.jpg
Manchester City wanaamini jaribio lao lenye thamani ya pauni milioni 60 (sh bilioni 174), litaweza kuishawishi Arsenal wawauzie mshambuliaji wao raia wa Chile, Alexis Sanchez (28) kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la msimu huu. Telegraph.

https://www.standard.co.uk/s3fs-public/thumbnails/image/2017/03/30/18/antonio-conte.jpg 
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amekwaruzana na uongozi wa timu hiyo kuhusiana na idadi ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa. Muitaliano huyo anataka kuwasainisha haraka wachezaji wazoefu na wanaouzwa bei chee. Times.

https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/08/nintchdbpict0003433441474.jpg?strip=all&w=960&quality=100
Barcelona wamesema dau lao la pauni milioni 90 (sh bilioni 261), kama ada ya uhamisho wa Ousmane Dembele (20) limekubaliwa na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani. Daily Express.

https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/01/632277292.jpg?w=620&h=444&crop=1
Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson amesema atajaribu kadri awezavyo kumshawishi mchezaji mwenzake Philippe Coutinho (25), kubaki klabuni hapo na kuipuuza ofa ya Barcelona. Daily Mirror.

http://img.bleacherreport.net/img/article/media_slots/photos/002/665/528/3b7e6e7da366dc9b2e3932f80c8c0d84_crop_exact.jpg?h=533&w=800&q=70&crop_x=center&crop_y=top
Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, Marco Asensio (21) ametaka kikao cha dharura baina yake na uongozi wa timu hiyo, baada ya kupokea ofa ya Arsenal. Sun.

https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/08/nintchdbpict000341578865-e1502564562227.jpg?strip=all&w=960&quality=100
Juventus wamesema wanavutiwa na mpango wa kumsajili kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere (25), ambaye hatima ya maisha yake ya mpira yako shakani Emirates. Daily Mirror.

http://e0.365dm.com/16/12/16-9/20/skysports-virgil-van-dijk_3860836.jpg?20161229154347
Beki mahiri wa Southampton, Virgil van Dijk (26) huenda akajiunga na aidha Chelsea au Manchester City kuliko Liverpool ambayo imekuwa ikimtaka. Hata hivyo, Southampton wanataka pauni milioni 70 (sh bilioni 203) kama ada ya uhamisho. Yahoo.

http://www.telegraph.co.uk/content/dam/football/2017/04/11/TELEMMGLPICT000125701801-xlarge_trans_NvBQzQNjv4BqPv2HyZ8xZ7FHfbDGTGwFDJ_mobP8C_LqfMoiS2i-b18.jpeg
Chelsea wanaamini kuwa wanaweza kumnasa winga wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain (23) kwa ada ya pauni milioni 35 (sh bilioni 101.5) kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la msimu huu. Evening Standard.

http://cdn.images.dailystar.co.uk/dynamic/58/photos/589000/620x/Davinson-Sanchez-609513.jpg
Maofisa wa Tottenham Hotspurs wamesafiri jana kwenda Amsterdam, kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Ajax ili wamsajili mlinzi wao wa kati, Davinson Sanchez (21). Ajax wanadai beki huyo anauzwa pauni milioni 36 (sh bilioni 104.4). Sky Sports.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search