Bilioni mbili zatumika ujenzi wa madarasa....soma habari kamili na matukio360...#share



Na mwandishi wetu,Kyela.

Kampuni ya ununuzi wa zao la Kokoa (Biolands ) Wilayani Kyela
Mkoani Mbeya imetumia zaidi ya Sh bilioni 2  kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 581 katika shule za msingi za halmashauri ya
Rungwe, Busokelo na Kyela.

Wadau wa elimu kutoka kampuni ya ununuzi wa zao la kokoa,(Biolands) kushoto Frank Neumann (katikati) Mkuu wa Mkoa Amos Makalla,(kulia) Antonie akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya Mkuu wa Shule katika shule ya Msingi Ngana Wilayani Kyela vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 23. Kulia ni Antonie Bernad.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bioland Tanzania, Antonie Bernad amesema hayo leo kwenye hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Ngana alipokuwa akimkabidhi mkuu wa mkoa, Amos Makalla vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya mwalimu mkuu na ukarabati wa majengo vyenye thamani ya Sh milioni 23.271  kati ya fedha hizo Sh 17 milioni zilitolewa na kampuni hiyo.

Amesema  wataendelea kuwekeza katika elimu lengo  kuisaidia
Serikali kuondokana na changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa

"Tutaendelea kuwekeza na kutoa elimu ya kilimo bora cha kisasa
kwa wakulima wa zao la kokoa ili kuwawezesha kupata mazao kwa wingi ,ili waweze kupata faida na kuendelea kuchangia shughuli za kijamii," amesema.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Amos Makalla ameagiza uongozi wa wilaya kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa kuhamasisha wananchi kupanda miche ya Kokoa ili waweze kunufaika kutokana na kuwepo kwa soko la uhakika.

"Wananchi jikiteni kwenye kilimo cha Kokoa. Na halmashauri wekeni mikakati mizuri ya kuwepo kwa vyama vya ushirika ambavyo vitasaidia wakulima kupata soko la uhakika hususan kuongeza thamani ya zao hili," amesema.


Makalla amesema wananchi sasa wanapaswa kutambua uchumi wao uko katika zao hilo na waongeze tija katika uzalishaji ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja au vikundi kupitia kampuni ya bioland, na vyama vya ushirika.

Ofisa elimu msingi wilaya ya Kyela, Palemon Ndarunguliye amesema kuna upungufu wa vyumba vya madarasa 568. Vilivyopo ni 724 ili kuweza kukidhi kuhudumia wanafunzi
1,288.

Amesema kufuatia changamoto hizo kwa mwaka wa fedha 2018/19 wametenga Sh 127 milioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 katika shule za msingi.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2017 halmashauri ,wananchi na wadau wa elimu walijenga vyumba vipya 168 na vyumba 69 vilikarabatiwa na zaidi ya Sh 2 .156 bilion zilitumika


Pia amesema kuna changamoto ya uhaba wa walimu  mahitaji ni 1,235 waliopo 976 na upungufu 449 sawa na asilimia 31.51.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search