Hawa hapa wajumbe wapya sekretarieti ya CCM Zanzibar....soma habari kamili na matukio360.....#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar imepitisha majina ya wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho visiwani Zanzibar, ambao watatumikia kwa kipindi cha miaka mitano.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdallah Juma Mabodi akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein
Sekratarieti hiyo imetangazwa leo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saddallah “Mabodi’ baada ya kumaliza kikao cha kamati hiyo kilichokuwa chini ya Uwenyekiti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, kilichofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar Mabodi amesema kuwa kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 68 ambao wote kwa pamoja waliweza kupitisha majina hayo.
Aliwataja wajumbe hao kuwa ni pamoja na Bakari Hamad Khamis anaekuwa Katibu wa Kamati Maalumu ya Oganaizesheni, Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi anakuwa Catherina Peter Nao, nafasi ambayo awali ilikuwa inashikiliwa na Waride Bakari Jabu.
Nafasi ya Katibu wa Idara ya Fedha na Uchumi inashikiliwa na Afadhali Tayb Afadhali , Mwalimu Kombo Hassan Juma anashika nafasi ya Katibu wa Idara ya Siasa na Uchumi na Uhusiano wa Kimataifa.
Aidha Mabodi aliwataja wajumbe wa Kamati ya Maadili na Uendeshaji kinidhamu ambao Mwenyekiti wake ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein na katibu ni Abdallah Juma Sadalla Mabodi.
Wajumbe wanaounda kamati hiyo ni Balozi Seif Ali Iddi, Mwalimu Kombo Hassan Juma na Ramadhan Shaibu Juma.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment