Maafisa jeshi la polisi wafundwa....soma habari kamili na matukio360....#share

 Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

JESHI la Polisi nchini limewataka maofisa wa jeshi hilo zaidi 50 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar waliopata mafunzo ya ushauri nasihi katika dawati la jinsia kutumia maarifa waliyopata kwa uadilifu na nidhamu ili kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Pichani ni walioshiriki mafunzo ya siku tano ya ushauri nasihi katika dawati la jinsia jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa jana jini Dar es Salaam na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Makao Makuu Benedict Wakulyamba alipokuwa akifunga mafunzo hayo ya siku tano yaliyodhaminiwa na Shirika la Utu wa Mtoto (CDF).

“Mafunzo haya kama jeshi la polisi tumekuwa tukiyahitaji na lengo kuu la taaluma hii ni kujiweka katika mazingira mazuri ya kuisaidia jamii, jambo la msingi ni uadilifu na nidhamu ya hali ya juu,” amesema SACP Wakulyamba.

Amesema lengo la kutumia maarifa hayo kwa uadilifu na nidhamu ni kutokana na kwamba wamepewa dhamana ya kusikia na kujua siri na changamoto za watu wengine hivyo wanatakiwa kuwasaidia wanajamii pasipo kutoa siri za matatizo yao nje.

“Itakuwa ni jambo la kushangaza kama utaona na kusikiliza tatizo la mtu na kulitangaza badala ya kusaidia na kulifanya kuwa siri baina yako na mwenye tatizo,” amesema.

SACP Wakulyamba ameeleza kuwa jamii imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za kisaikolojia hivyo moja ya majukumu ya maofisa hao ni kupenyeza elimu waliyopata ili kusaidia kuzauia matatizo ambayo yanaweza kuzuilika.

Kwa upende wake Meneja Mipango wa CDF Dorothy Ernest, amesema kuwa tatizo la ukatili wa kijinsia na watoto nchini bado ni kubwa na kwamba wamekuwa wakipambana nalo kwa muda mrefu na kueleza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto hiyo.

“Mafunzo haya yatasaidia kuboresha madawati ya jinsia na watoto nchini ili kuutokomeza ukatilii huu wa kijinsia na tutaendelea kushirikiana na jeshi la polisi,” amesema.

Ameongeza kuwa katika mwaka huu wataendelea kuboresha madawati ya jinsia kwenye maeneo mbali mbali nchini hususani katika kupata taarifa ambapo alisema kila mmoja akiwajibika tatizo hili linaweza kutokomezwa.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Inspekata Amina Daffa kutoka Mkoa wa Kipolisi Ilala jijini Dar es Salaam, ameshukuru kwa mafunzo hayo na kwamba watayatumia vizuri katika kuhakikisha wanaisaidia jamii ili kuondokana na tatizo la ukatili wa kijinsia na changamoto mabli mbali zinazoikabili.





About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search