Makonda: Waliodhulumiwa nyumbani, viwanja warejee Februari 10....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
WANANCHI waliosikilizwa na wanasheria katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Februari 10, 2018 wametakiwa kufika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia Saa moja asubuhi ili kupatiwa mrejesho wa malalamiko yao.
Paul Makonda
Mwenasheria wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo, Fabiola Mwingira amesema idadi ya wananchi waliojitokeza ni kubwa tofauti na matarajio yao lakini wamejitahidi hadi sasa zaidi ya wananchi 3,000 wamepatiwa huduma..
"Zaidi ya wananchi 3000 wamepatiwa huduma ya msaada wa kisheria ndani ya siku tano kutokana na kudhulumiwa mali zao lakini kutokana na idadi kuwa kubwa muda wa kusikilizwa umeongezwa hadi kesho," amesema Fabiola
Amesena mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameongeza siku za kusikiliza malalamiko na madai ya waliodhulumiwa ili kuhakikisha wananchi wote waliofika wanasikilizwa na kuhudumiwa.
Hatua hiyo ya Makonda imefikiwa kutokana na idadi kuwa kubwa ya wananchi waliojitokeza kupata msaada wa kisheria.
Taarifa za kuongezwa kwa muda zimepokelewa kwa shangwe na wananchi ambapo wamemsifu Makonda kwa kutanguliza utu mbele kwa kuhakikisha wanyonge wanaipata haki yao waliyotaabika kuitafuta kwa miaka mingi.
No comments:
Post a Comment