Magufuli amkabidhi bajaj mlemavu aliyemuahidi....soma habari kamili na matukio360...#share


Katibu wa Rais Ngusa Samike na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa wakimwongoza mlemavu wa maungo Yusuf Abdulrahman Ndemanga kwenye Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais John Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018.

Katibu wa Rais Ngusa Samike akimkabidhi  mlemavu wa maungo Yusuf Abdulrahman Ndemanga Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais  John  Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018. Kulia ni mkewe  Ndemanga, Hawa Mohamed.


Mlemavu wa maungo  Yusuf Abdulrahman Ndemanga na mkewe Hawa Mohamed Wakiondoka na Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais John  Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018. 


Rais John Magufuli akimsikiliza Yusuph Abdulrahman Ndemanga ambaye ni mlemavu wakati alipomkuta ndani ya jengo la abiria lililopo upande wa Magogoni kabla ya kuvuka na Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam Agosti 25, mwaka jana. Bw. Ndemanga alimuomba Rais msada wa kupatiwa Bajaji ili ajimudu kiusafiri na kiuchumi.




Picha na IKULU

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search