Mhh! Muhuhubiri asema wanawake ''chanzo cha uovu''.....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
MUHUBIRI, Nicolas Niyibikora wa nchini Rwanda huenda akaingia matatani mbele ya vyombo vya sheria baada ya kuwaita wanawake ''chanzo cha uovu''
Muhubiri huyo wa kanisa la Seventh Day Adventist aliwaambia wanawake kwamba hawapendwi na Mungu wakati wa matangazo ya idhaa ya redio ya Amazing Grace mwezi Januari akionya kuwa ''hakuna lolote jema linaloweza kupatikana kutoka kwa wanawake''.
''Unaposoma Biblia , ni nani aliyeleta dhambi duniani''? Aliuliza na kuongeza, ''sio mwanamume''.
Tayari mahubiri hayo yamewakasirisha wanaharakati huku wale wanaounga mkono usawa wa kijinsia wakiitisha mkutano na vyombo vya habari na kuonya kuwa maneno kama hayo yanaweza kusababisha chuki na mzozo miongoni mwa raia wa Rwanda iwapo hakuna hatua ya haraka itachukuliwa , kulingana na gazeti la Rwanda la New Times.
Kundi la kutetea haki za wanawake liliwasilisha malalamishi yake katika tume ya udhibiti wa vyombo vya habari ambayo inatarajiwa kukutana ili kuzungunmzia kuhusu suala hilo wiki ijayo.
Afisa mkuu, Emmanuel Mugisha aliambia gazeti la New Times kwamba kuna uwezekano idhaa hiyo ikajieleza.
Hata hivyo Kanisa la Seventh Day nchini Rwanda limefanya juhudi za kujitenga na Niyibikora ambaye wanasema alipigwa marufuku kwa miaka ,mitano.
No comments:
Post a Comment