Mke wa Trump JR apelekwa hospitali baada ya kupewa unga....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
MKE wa mtoto wa rais Trump, Trump Jr, Vanessa Trump, amepelekwa hospitalini kama njia ya kuchukua tahadhari baada ya kufungua bahasha yenye unga mweupe.
Trump JR akiwa na familia yake ya watoto watano
Barua hiyo ilikuwa imetumwa kwa Donald Trump Jr, mtoto wa kwanza wa kiume wa Rais Trump, katika nyumba yake huko Manhattan.
Bi Trump na watu wengine waliokuwa eneo hilo waliondolewa na wazima moto na kisha kupelekwa hospitalini.
Polisi wa mjini New York waliiambia BBC kuwa waliufanyia uchunguzi unga huo na haukuwa na madhara.
Walisema kuwa Bi Trump hakuonekana kuthiriwa na unga huo.
Trump baadaye aliandika katika mtandao wa Twitter na kukashifu kitendo hicho.
Kulingana na kituo cha CBS mjini New York mama yake Vanessa Trump, alishika barua hiyo kabla ya Vanessa kuifungua.Walinzi wa rais wanasema wanaichunguza barua hiyo.
Donald Trump Jr ambaye anafanya biashara ya baba yake, alimuoa Vanessa Kay Haydon Novemba mwaka 2005 katika eneo la starehe la Trump huko Forida.
Shangazi ya Trump Jr, jaji Maryanne Trump Barry, alisimamia sherehe hiyo. Kabla ya kuolewa na Trump Jr, Vanessa alikuwa mwanamitindo huko New Nork.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search