Watano wafariki, sita wajeruhiwa katika ajali...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Tanga

WATU watano wamefariki papo hapo na wengine sita kujeruhiwa katika ajali iliyotokea jana katika barabara ya Segera- Kabuku wilayani Hadeni mkoani Tanga.


SIMANZI: Hivi ndivyo ajali ya Basi la AJ_Safari ilovyotokea ,Baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Hiace katika kijiji cha Kabuku Wilayani Handeni Mkoani Tanga.

Kaimu kamanda mkoa wa Tanga  Leon Rwegasira ameiambia matukio360 kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili, Hiace na basi kubwa aina ya Youtong.

Amesema dereva wa hiace ni miongoni mwa waliofariki na kwamba wanamshikiria dereva wa basi ambaye ni mkazi wa Dar es salaam.


"Hadi sasa bado hatujajua chanzo cha ajali, tulichofanya ni kuokoa majeruhi na hali zao zikitengemaa tutawauliza majina yao, wanapoishi na sababu za ajali. Lakini hadi ninavyoongea watano wamefariki na sita wamejeruhiwa," amesema Rwegasira

Amesema basi hilo lilikuwa linatoka Tanga kwenda Dar es salaam


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search