Mwanasheria mkuu Kenya ajiuzulu....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
MWANASHERIA mkuu wa Kenya, Profesa Githu Muigai amejiuzulu baada ya kuhudumu kwa miaka sita na nusu.
Profesa Githu Muigai
Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Profesa Githu kwa huduma zake na sasa jaji Paul Kihara Kariuki atachukua mahala pake.
"Nimepokea kwa majuto uamuzi wa mwanasheria mkuu Githu Muigai . Namshukuru kwa huduma yake katika kipindi cha miaka sita na nusu. Nimemteua jaji Paul Kiharara Kariuk''i , Rais Uhuru Kenyatta alichapisha katika mtandao wake wa Twitter.
Kabla ya uteuzi wake kuwa mwanasheria mkuu profesa Muigia alikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya mawakili ya Mohammed Muigai na amekuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na ubaguzi wa rangi.
Alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha sheria cha Columbia mjini New York . Kutoka 1984 alikuwa mwanfunzi katika chuo cha kusomea uanasheria nchini Kenya .
Vilevile alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi .
Akiwa mshauri wa serikali katika maswala ya kisheria, Githu Muiga atakumbukwa kwa kuleta sheria za mageuzi katika timu ya uchaguzi nchini Kenya siku chache tu kabla ya uchaguzi kufanyika.
Katika sheria hiyo kamishna yeyote yule katika tume ya uchaguzi alipewa nguvu za kumtangaza mshindi wa uchaguzi iwapo mwenyekiti wa tume hiyo hayupo.
Sheria hiyo ilizua pingamizi kutoka kwa upinzani pamoja na jamii ya kitaifa waliodai kuwa serikali haiwezi kufanya mabadiliko ya sheria wakati ambpo uchaguzi mkuu unakaribia.
No comments:
Post a Comment