Mchezaji Juma Nyoso kifungoni tena....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu nchini (TFF) imetangaza kumfungia michezo mitano na faini ya sh.milioni
1 beki wa Kagera Sugar Juma Nyoso kwa
kosa la kupiga shabiki baada ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Simba kwenye
uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Juma Nyoso
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa habari wa TFF
Clifford Ndimbo, uamuzi huo umefikiwa baada ya shauri lake kufikishwa kwenye
kamati hiyo.
“Kamati imemtia hatiani Juma Nyoso
kupitia kanuni za ligi kuu na katiba ya TFF lakini ilipokea taarifa za nyuma za
Nyoso kwamba aliwahi kuadhibiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Kwa hiyo kamati
imemfungia Nyoso mechi tano pamoja na faini ya shilingi 1,000,000 (milioni
moja),” amesema Ndimbo.
Kwa mujibu wa Ndimbo Nyoso alituhumiwa kumpiga shabiki baada ya
kumalika kwa mchezo kinyume na kanuni za ligi kuu zinazozungumzia mchezo wa
kiungwana.
Hivyo kamati ilipitia ripoti ya kamishna
wa mchezo ambayo imeeleza tukio la kupishana kwa Nyoso na shabiki ambaye alikuwa
amebeba vuvuzela na mchezaji huyo akaonekana kusimama na kuanza kumpiga shabiki
kwa kutumia kiatu na baadaye akamuinamisha na kuanza kumpiga kwa kutumia goti.
Kamati ilimwita Nyoso kujitetea, kwa
upande wake alikataa madai hayo ya kumpiga shabiki. Alisema alichofanya ilikuwa
ni kumkunja tu shabiki huyo lakini hakumpiga.
No comments:
Post a Comment