Serikali yapata mrahaba bilioni mbili....soma habari kamili na matukio360....#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
SERIKALI imepata mrahaba wa (Final Royalty) wa sh. bilioni 2
sawa na dola za kimarekani 816, 471.52 pamoja na ada ya ukaguzi kiasi cha dola
za Marekani 136,078.59.
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko.
Pia imesema kufuatia merekebisho ya sheria ya madini yaliyofanyika
kupitia ‘The written Laws’ (Miscellaneous Amendments) Act, 2017 na kufuatia
kusainiwa kwa kanuni za madini za mwaka 2018 na waziri wa madini sasa vibali vya
usafirishaji wa madini nje (export permits) ya nchi vitaombwa kwa tume ya
madini na kusainiwa na kaimu katibu mtendaji wa tume ya madini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, amesema mrahaba huo unatokana na mnada wa
tatu wa Februari 2 hadi 9, 2018 wa mauzo ya almasi kutoka mgodi wa Mwadui
unaomilikiwa na kampuni ya Williumson Diamonds Limited uliofanyika mjinin
Antwerp, nchini Ubelgiji.
“Katika mnada huo, jumla ya karati 54,094.47 ziliuzwa kwa
thamani ya dola za Marekani 13,607,858.72 sawa na sh.bilioni 30.6 ambapo jumla
ya kampuni 145 zilishiriki katika mnada na kuwasilisha zabuni zao za ununuzi na
zabuni 1,019 zilizowasilishwa katika
mnada huo,” amesema Biteko.
Aidha amesema mrahaba wa awali (Provisional Royalty)
uliolipwa kutokana na uthaminishaji wa awali kabla ya mauzo ni dola za Marekani
674,941.78, ada ya Clearance na Inspection dola za Marekani 112,490.30 ambapo
jumla yake ni dola za Marekani 787,532.08 sawa n ash. Bilioni 1.7.
Katika hatua nyingine Biteko amesema kuwa ujenzi wa ukuta
kwenye mgodi wa Mererani wenye urefu wa kilometa 24.5 upo katika hatua za mwisho
kukamilika.
Hivyo kutokana na hatua hiyo kuanzia Februari 19, 2018 mamlka
ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kushirikiana na wataalam wa wizara ya
madini wataanza zoezi la utoaji wa vitambulisho vya Uraia kwa wananchi wa eneo
husika.
Amesema zoezi hilo limelenga kuhakikisha kuwa wananchi watakaoingia
katika eneo la usajili na utoaji wa vitambulisho wawe wanatambulika kwa kuwa na
vitambulisho vya uraia kwani lengo kuingilia katika eneo hilo la migodi ya Tanzanite
litakuwa moja tu. Hivyo, yeyote asiyekuwa na kitambulisho hicho hataruhusiwa
kuingia eneo la mgodi.
No comments:
Post a Comment