SERIKALI:Kila mwezi wanafunzi sekondari wapimwe ujauzito...soma habari kamili na matukio360....#share
Na mwandishi wetu, Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya sasa ameagiza kila mwezi wanafunzi wa kike wa shule za sekondari wapimwe ujauzito.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na wanafunzi na wananchi katika Shule ya Sekondari Madibira alipofanya ziara ya kikazi.
Agizo hilo limetokewa na mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla katika ziara yake ya
kukagua miundombinu ya vyumba vya madarasa sita na bweni la wanafunzi
wa kiume katika Shue ya Sekondari Madibira Wilayani Mbarali
"Sera ya elimu bure, pia inalenga kuhakikisha mtoto wa kike anapata
elimu sasa wasimamizi wa wanafunzi katika shule za bweni muwe na
utaratibu wa kuwapima kila mwezi isije kutokea wanasoma wakiwa
na ujauzito," amesema.
Amesema utaratibu huo ulikuwapo miaka ya nyuma na sasa ameagiza uanze kuanzia leo.
Pamoja na mambo mengine amewataka wanafunzi wa kike kuwapuuza wanaume wanaowalaghai kwa kuwapa pesa na vitu mbalimbali ili kujenga uhusiano.
"Muwapuuze vijana wanaowalaghai wanawakatisha ndoto zenu za kuwa
mawaziri,wakuu wa mikoa simamieni elimu ndio msingi mkuu wa maisha
yenu na ndio urithi wa baadaye," amesema
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune amesema atasimamia utekelezaji wa agizo
hilo na kuwaagiza wasimamizi wa watoto katika shule za bweni
kutekeleza ili kupunguza mimba za utotoni kwa watoto wa kike.

No comments:
Post a Comment