Siha tayari kwa uchaguzi....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu Siha-Kilimanjaro
ZIKIWA zimebakia siku mbili kabla ya kufanyika uchaguzi mdogo wa marudio wa majimbo mawili na kata nane, maandalizi katika jimbo la Siha na udiwani katika kata tatu za jimbo hilo mkoani Kilimanjaro yamekamilika.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Siha, Valerian Juwal
Msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo, Valerian Juwal amesema vifaa vyote kutoka Nec kwa ajili ya uchaguzi vimepokelewa na mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi yanaendelea.
Akizungumzia kuhusu kampeni zinazoendelea kwa Vyama vinavyoshiriki uchaguzi, Juwak amesema kumekuwepo na vitendo vinavyokiuka maadili ya uchaguzi ingawa kamati ya maadili imekuwa ikichukua hatua kwa mujibu wa taratibu.
Ametaja baadhi ya vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ambavyo vimewasilishwa katika Kamati ya Maadili kuwa ni pamoja na baadhi ya wanachama wa Vyama vya siasa kufanya Maandamano baada ya mikutano, baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Vyama hivyo kutoa kauli za vitisho na lugha za maudhi dhidi ya Vyama vingine.
Msimammizi huyo wa Uchaguzi ambaye amewataka wakazi wa Jimbo la Uchaguzi la Siha kujitokeza siku ya Uchaguzi ili kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wao na kutahadharisha watu au kikundi chochote cha watu watakaojaribu kuvuruga Uchaguzi huo.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment