Ukuta madini Tanzanite wakamilika kwa asilimia 90....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, 
UKUTA mrefu unaozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite katika eneo la Mererani, umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
Geti kuu la kuingia kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite likiendelea kujengwa 
Ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu, umejengwa kufuatia agizo lililotolewa na Rais John Magufuli, kama jitihada za kudhibiti na kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.
Tayari wakuu wa vyombo vya usalama, wametembelea eneo hilo, kuukagua ukuta huo uliojengwa kwa gharama za kiTanzania isiyozidi bilioni 6.
Na kusisitiza kuwa lengo la kujengwa kwake ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.

Ukuta mrefu ukizunguka eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite
Wakitoa taarifa kwa viongozi wa ulinzi, wataalamu waliojenga ukuta huo, wanasema licha ya kufanikisha ujenzi huo, changamoto mbalimbali walikutana nazo ikiwemo hatari inayo ukabili ukuta huo, kutokana na wachimbaji kulipua baruti, karibu na ukuta, hivyo kusababisha hatari za kuharibika haraka.
Ugumu wengine walioupata ni uchimbaji katika maeneo yenye miamba.
Kwa upande wao, wakizungumzia usalama baada ya kukagua eneo hilo, wamezungumzia uadilifu katika kulinda eneo hilo.
Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo amesema ukuta uko imara na kwamba hatua ya pili itafuata katika kuuboresha zaidi.
Amesisitiza kuwa ulinzi unahitaji uzalendo zaidi kutokana na Watanzania wakati mwingine kuwa ndio wanaohujumu mali za nchi.
Sehemu ya ukuta unaozunguka eneo la uchimbaji madini ya Tanzanite
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro amesema jambo kubwa ni wananchi kuwa na uelewa kwa nini ukuta huo umejengwa.
Baada ya kukamilika kwa awamu hiyo ya ujenzi, awamu ya pili itafuata kuboresha baadhi ya maeneo na kuweka vifaa zaidi vya kiusalama.
Rais wa Tanzania John Magufuli anatarajiwa kuuzindua rasmi ukuta huo, utakapokamilika kwa asilimia mia moja.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search